Kuandaa kitalu cha miche ya pilipili

Tazama video hapo juu kujifunza zaidi kuhusu uandaji wa kitalu cha miche ya pilipili.
Kuandaa kitalu cha miche ya pilipili kwanza andaa sehemu ya kuoteshea kwa kulima vizuri na kusawazisha, kisha chora mitaro isiyo na kina kirefu ukitumia kijiti, mitaro inafaa kuwa sambamba, mitaro iachane kwa sentimita 15 mtaro mmoja kwenda mwingine, hakikisha umeandaa mbegu bora, weka mbegu chache kwenye kila mtaro hakikisha unaacha nafasi ya kutosha kati ya kila mbegu, usiweke mbegu nyingi kwa sababu utaishia kuwa na miche mirefu myembamba isiyothabiti, mbogamboga nyingi huwa na mbegu ndogo zinazofaa kupandwa juujuu ya ardhi, rashia udongo laini ili kufunika mbegu, ukiwa umetumia mbegu bora karibu kila mbegu itaota.
Youtube channel    Subscribe here