Kilimo cha Mahindi ya Kuchoma Tanzania
Dhana ya kulima mahindi na kuuza mabichi kwenye soko kabla hayajafikia hatua ya unga mgumu inajulikana kama kilimo cha mahindi ya kuchoma au uzalishaji wa mahindi mabichi, Kwa kawaida zao la mahidi hudumu kwa takribani siku 90 hadi 120 shambani inategemeana na aina ya mbengu lakini kwa mahindi ya kuchoma ni takribani siku 60 hadi 75 tu yanatoka shambani, Kilimo hiki kinamruhusu mkulima kuwa na angalau misimu miwili kabla ya msimu wa mvua kama analima kwa umwagiliaji.
Ni dhahiri kuwa kilimo cha mahindi mabichi ni mradi wa faida ukizingatiwa na kutiliwa maanani, kwenye ekari moja kuna wastani wa miche 17, 700 hapo utakua umepanda mbegu mbili kwenye kila shimo kwa umbali wa Sentimita 75 kwa 60, sasa baada ya kuwekeza pesa yako kwa vile unalima kibiashara ni matumaini utafuata hatua zote za kilimo bora cha mahindi, sasa ni muda wa kuingia sokoni, Tunakadiria kuwa ulivuna mahindi 15,000 tu, yaani kila mche upate hindi moja tu bora, achilia mbali habari ya mahindi kubeba mawili mawili kila mche na bado tumepunguza idadi miche kutoka 17,700 hadi miche 15,000 sass unajua una kiasi gani hapo?
Ni hesabu ndogo sana, chukua Tsh. 150/= zidisha kwa 15,000. Tsh. 150/= ni bei ya kuuzia shambani hapo utapata milioni mbili laki mbili na elfu hamsini Tsh. 2,250,000/= basi toa Tsh. 1,000,000/= milioni moja kama gharama, hapo unapata faida ghafi ya milioni moja na laki mbili na hamsini, hiyo ni ekari 1 na ni makadirio ya chini kabisa.
Youtube channel ➭ Subscribe here