Maarifa ni muhimu katika kuendeleza jambo lolote, maarifa sahihi yakikosekana unaweza ukakosa ufanisi kwenye jambo unalofanya.
Ili ufanikiwa katika kilimo unahitaji maarifa sahihi juu ya kilimo cha zao husika, Wakulima wengi wadogo hukimbilia kujua gharama za uzalishaji na faida ni wakulima wachache wanatumia muda kujifunza juu ya zao ambalo wanataka kulima, kuwa na fedha ya kutosha haikufanyi wewe kufanikiwa katika kilimo japo inaweza kukuwezesha kufanya shughuli za kilimo kwa urahisi zaidi kwa vile rasilimali fedha ni muhimu pia katika kilimo.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kabla ya kuanza shughuli zako za kilimo jaribu kutafuta maarifa sahihi juu ya zao unalotaka kulima:
Mambo muhimu ambayo unapaswa kuyajua nje ya gharama za uzalishaji ni haya yafuatayo:
☑️ Ardhi (udongo) unaoendana na zao husika.
☑️ Mbegu bora
☑️ Msimu mzuri wa kuzalisha
☑️ Mbinu bora za uzalishaji wa zao husika
☑️ Matumizi sahihi ya mbolea
☑️ Magonjwa na wadudu waharibifu wa zao husika
☑️ Upatikanaji wa viuatilifu
☑️ Mzunguko wa mazao shambani
☑️ Masoko ya zao husika
Kwahiyo ni muhimu angalau kujifunza ili kupata maarifa sahihi kwenye zao hilo unalotaka kulima ili walau kupata mwanga wa kile unachokwenda kufanya.
"Kukosa maarifa sahihi ni kutaka kuangamia"
Youtube channel ➭ Subscribe here